Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 241

Al-Baqara 2:241

البقرة

وَلِلْمُطَلَّقَـٰتِ مَتَـٰعٌۢ بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُتَّقِينَ

Maana

Na wanawake waliotalikiwa wapewe cha kuwaliwaza kwa wema. Hii ni haki juu ya wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa mujibu wa Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu. [241]

[241] Na wanawake walio pewa T'alaka baada ya kuingia harusi wana haki wapewe mali ya kuwaliwaza. Wapewe kwa wema, kwa kadiri ya utajiri na umasikini wa mume. Kumcha Mwenyezi Mungu kunawajibisha hayo, na pia watu wa Imani wanalazimika na hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanawake waliotalikiwa wanastahiki wapewe kiliwazo cha mavazi na matumizi kwa mujibu wa mpango unaojulikana na kupendekezwa kisheria. Hiyo ikiwa ni haki juu ya wale wanaomuogopa Allah Mtukufu katika amri Zake na Makatazo Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net