Al-Baqara 2:240
البقرةوَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَٰجِهِم مَّتَـٰعًا إِلَى ٱلْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِى مَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanawaacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumbani. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika yale waliyojifanyia wenyewe kwa wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [240]
[240] Wanao kufa miongoni mwenu wakaacha wake zao, Mwenyezi Mungu ameusia hao wanawake wafiwa wabaki nyumbani mwa waume zao muda wa mwaka mzima kwa maliwaza na kuwaondolea ukiwa. Wala hana haki yeyote kuwatoa. Wakitoka kwa khiari yao kabla ya mwaka kwisha basi hamna dhambi nyinyi wenye madaraka mkiwaachilia wajitendee wenyewe wapendalo kwa lisio vunja Sharia tukufu. Na mt'iini Mwenyezi Mungu katika hukumu zake, na tendeni Sharia alizo kutungieni kwani Yeye ni Muweza wa kumuadhibu anaye kwenda kinyume na amri yake, na Yeye ni Mwenye hikima iliyo pita ukomo. Hakuamrishini ila lenye maslaha yenu ijapo kuwa hikima yake imepindukia ujuzi wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waume wanaofariki na wakaacha wake baada yao, inawalazimu waume hao wawekee wasia hao wake zao kwamba waliwazwe mwaka mzima kuanzia siku ya kufariki, kwa kupewa makao katika nyumba ya mume, bila ya kutolewa na mawarithi kwa muda wa mwaka. Hilo likiwa ni maliwazo kwa yule mke na ni wema kwa aliyefariki. Na iwapo wanawake hao waliofiliwa watatoka, kwa hiyari yao kabla mwaka kumalizika, basi hamna makosa, nyinyi warithi, katika hilo. Pia, hakuna makosa kwa hao wanawake kwa kitendo chao cha halali walichojifanyia nafsi zao. Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika amri Zake na Makatazo Yake. Aya hii, hukumu zake zimeondolewa kwa neno Lake Allah Mtukufu, «Na wale wanaofariki kati yenu na wakaacha wake zao, (Basi wake hao) wajizuie nafsi zao Miezi minne na siku kumi»(2:234).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net