Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَٰجِهِم مَّتَـٰعًا إِلَى ٱلْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِى مَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ 240
{240} Inajulikana kwa wafasiri wengi kwamba Aya hii tukufu ilifutwa na Aya ya kabla yake, ambayo ni kauli yake Mola Mtukufu. "Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanawaacha wake, basi wake hawa wazizuie nafsi zao miezi minne na siku kumi." Na kwamba jambo lilikuwa kwamba mke alilazimika kujizuia mwaka mzima, kisha likafutwa kwa miezi minne na usiku kumi. Na wanajibu kuhusu kutanguliza Aya iliyofuta (mbele ya Aya iliyofutwa) kuwa huko ni kutangulia tu katika mahali (pa Aya katika Qur-ani), na si katika kuteremka kwake. Kwa sababu, sharti la Aya yenye kufuta ni kwamba ije nyuma ya ile aliyofutwa. Na kauli hii haina ushahidi juu yake. Na mwenye kuzitafakari Aya mbili hizi, itamdhihirikia kuwa ile kauli nyingine kuhusu Aya hii ndiyo sahihi. Na kwamba Aya ya kwanza yenye uwajibu wa kujizuia miezi minne na usiku kumi ni jambo la lazima kwa mwanamke. Na ama katika Aya hii, ina wasia kwa jamaa za maiti kwamba, waendelee kubaki pamoja na mke wa maiti wao kwa muda wa mwaka mzima ili kupoza fikira zake na kumfanyia wema maiti wao. Na ndio maana akasema, "na wausie kwa ajili ya wake zao." Yani ni wasia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa jamaa za maiti kwamba, watafute ushauri kutoka kwa mkewe, na wampe cha kumliwaza, na wasimtoe nje. Na akitaka, basi ataendelea kukaa katika wasia wake, na akipenda kuondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yake. Na ndiyo maana akasema, "na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika waliyojifanyia wenyewe kwa wema." Yani kama vile kujirembesha na (kuvalia) mavazi (mazuri), lakini sharti ni kwamba yawe hayo kwa wema ambao hauyatoi nje ya mipaka ya dini na kuzingatia. Na akahitimisha Aya kwa majina haya mawili makubwa yanayoashiria ukamilifu wa nguvu yake na ukamilifu wa hekima yake. Kwa sababu, hukumu hizi zilitokana na nguvu yake, na zinaashiria ukamilifu wa hekima yake, kwa kuwa iliziweka katika mahali pake panapozifaa.