Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 239

فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَآ أَمِنتُمْ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا۟ تَعْلَمُونَ 239

{239} Na kauli yake, "na mkiwa na hofu" kimefutwa kinachohofiwa; ili (Aya) ienee hofu ya adui na mnyama mwitu na kupotea kwa yale ambayo mja atadhurika kwa kupotea kwake. Basi swalini, "hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda" juu ya farasi, ngamia na vipando vinginevyo. Na katika hali hii haimlazimu (mtu) kuelekea kibla. Basi hii ndiyo namna (sifa) ya swala ya mwenye udhuru ya hofu. Na amani itakapotokea, ataswali swala kamili. Na inaingia katika kauli yake, "na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu," kuzikamilisha swala. Na inaingia humo pia kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa kumshukuru juu ya neema ya amani, na juu ya neema ya kufundisha (waja) yale ambayo yana furaha ya mja ndani yake. Na katika Aya hii tukufu, kuna fadhila ya elimu. Na kwamba yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfundisha yale ambayo hakuwa anayajua amkumbuke Mwenyezi Mungu kwa wingi. Na pia ndani yake kuna kujulisha ya kwamba kumkumbuka kwa wingi ni sababu ya kufundishwa elimu zingine. Kwa sababu, kushukuru kumefungamanishwa na kuzidishiwa. Kisha yeye Mtukufu akasema: