Al-Baqara 2:239
البقرةفَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَآ أَمِنتُمْ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا۟ تَعْلَمُونَ
Na mkiwa na hofu, basi (swalini) hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama alivyowafunza yale ambayo hamkuwa mnayajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyo kufunzeni yale mliyo kuwa hamyajui. [239]
[239] Ukikufikieni wakati wa Swala nanyi mko katika khofu basi msiache kusali, bali swalini kama muwezavyo, ikiwa huku mnakwenda kwa miguu au mmepanda kipando. Ikiondoka khofu swalini kwa kutimiza nguzo zote kama mlivyo jifunza, mkimkumbuka Mwenyezi Mungu katika Swala na mkimshukuru kwa aliyo kufunzeni, na kwa kukujaalieni kuwa katika amani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iwapo mtawaogopa maadui wenu, swalini swala ya khofu, mkiwa mwatembea au mumepanda, kwa namna yoyote ile mnayoiweza, hata kama ishara, au hata kama hamkuelekea kibla. Na pindi khofu yenu itakapokwisha, swalini swala ya amani na mumtaje Allah Mtukufu humo. Wala msiipunguze kwakuitoa kwenye namna yake ya asili. Na mshukuruni Allah Mtukufu kwa kuwafundisha mambo ya ibada na hukumu ambayo hamkuwa na ujuzi nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net