Al-Baqara 2:238
البقرةحَـٰفِظُوا۟ عَلَى ٱلصَّلَوَٰتِ وَٱلصَّلَوٰةِ ٱلْوُسْطَىٰ وَقُومُوا۟ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ
Zilindeni Swala, na hasa Swala ya katikati. Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Zilindeni Swala, na khasa Swala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea). [238]
[238] Fanyeni hima katika kusimamisha Swala zote na kuzidumisha. Na fanyeni hima kuwa Swala yenu iwe ni Swala bora kwa kuzitimiza nguzo zake na kumsafia niya Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu katika Swala. Na timizeni ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mkumbukeni kwa usafi wa moyo na kunyenyekea Utukufu wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zihifadhini, enyi Waislamu, Swala tano zilizofaradhiwa kwa kudumu nazo katika kuzitekeleza kwa nyakati zake, mashariti yake, nguzo zake. Na mhifadhi swala iliyo katikati ya swala hizo, nayo ni Swala ya Alasir. Na simameni katika Swala zenu hali ya kumtii Allah Mtukufu, kumnyenyekea na kumdhalilikia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net