Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 237

Al-Baqara 2:237

البقرة

وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّآ أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَا۟ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ عُقْدَةُ ٱلنِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوٓا۟ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا۟ ٱلْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa, na tayari mmeshawakatia mahari mahususi, basi wapeni nusu ya mahari mliyowakatia. Isipokuwa ikiwa wanawake wenyewe watasamehe, au amesamehe yule ambaye fundo la ndoa liko mkononi mwake. Na mkisamehe ndiyo kuwa karibu zaidi na ucha Mungu. Wala msisahau fadhila zilizo baina yenu. Hakika, Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkiwapa T'alaka kabla ya kuwagusa, na mmekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeni nusu ya mahari mlio agana, isipo kuwa ikiwa wanawake wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake awe amesamehe. Na kusameheana ndiko kulio karibu zaidi na uchamngu. Wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. [237]

[237] Pindi mkiwapa T'alaka wanawake kabla ya kuingia harusi lakini baada ya kwisha wafikiana mahari, basi ni haki yao hao wat'alaka wapewe nusu ya mahari, ila wenyewe kwa ridhaa yao wakikataa kuchukua kitu. Na wao pia hawapewi zaidi ya nusu ila waume nafsi zao wakasamehe na wakatoa mahari yote kaamili. Na kila mmoja wapo kusamehe ndio ubora zaidi na ni kumridhisha zaidi Mwenyezi Mungu, na ndio mambo yanavyo elekea kwa wachao Mungu. Basi msiache huu mwendo wa kusameheana. Na kumbukeni kuwa kheri iko katika kufadhiliana na kufanyiana ihsani. Hayo ndiyo yanayo pelekea kupendana baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema dhamiri zenu na atakulipeni kwa fadhila mzitendazo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo mtawataliki wanawake, baada ya kufunga ndoa nao na kabla hamjawaingilia, na mkawa mumejilazimisha kuwapa kiasi maalumu cha mahari, basi inawapasa muwape nusu ya mahari mliyokubaliana, isipokuwa iwapo watalaka hao watasamehe na kuiacha ile nusu ya mahari iliyopasa wapewe, au iwapo mume atasamehe kwa kumuachia mtalaka mahari yote. Na kusamehe kwenu, enyi wanaume na wanawake, ni jambo lililo karibu zaidi na kumcha Allah Mtukufu na kumtii. Wala msisahau, enyi watu, fadhila na wema kati yenu ambao ni kutoa ambacho si wajibu kwenu kukitoa na kusameheana. Hakika Allah Mtukufu, kwa mnayoyafanya, ni mwenye kuona. Anawahimiza kufanya kheri na kuwasogeza kufanya wema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net