Al-Baqara 2:236
البقرةلَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا۟ لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى ٱلْمُوسِعِ قَدَرُهُۥ وَعَلَى ٱلْمُقْتِرِ قَدَرُهُۥ مَتَـٰعًۢا بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُحْسِنِينَ
Hakuna ubaya wowote juu yenu mkiwataliki wanawake ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari yao. Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kwa kiwango awezacho na mwenye dhiki kwa kiwango awezacho, maliwazo kwa wema, ni haki juu ya watendao mema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana ubaya kwenu mkiwapa T'alaka wanawake ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari yao. Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kadiri awezavyo na mwenye dhiki kadiri awezavyo - maliwaza kwa mujibu wa dasturi kuwa ni haki juu ya watendao mema. [236]
[236] Wala hapana dhambi kwenu enyi waume, wala hapana mahari juu yenu mkiwaacha wake kabla ya kuingia harusi na kabla hamjawatajia kiasi cha mahari. Lakini wapeni zawadi kama kuwapoza kuwapunguzia machungu ya moyo. Na hicho mnacho toa kiwe cha kuridhisha na kupendeza moyo. Tajiri atoe kwa kadiri ya wasaa wake, na fakiri kwa kadiri ya hali yake. Na zawadi hiyo ni katika a'mali za kheri wanazo jilazimisha nazo watu wenye muruwa na watu wa kheri na ihsani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna dhambi juu yenu, enyi wanaume, iwapo mtawataliki wanawake baada ya kufunga ndoa nao na kabla ya kuwaingilia au kuwatajia mahari. Hivyo basi, waliwazeni kwa kuwapa kitu chenye kuwanufaisha kwa kuwaliwaza na kuwaondolea maudhi ya talaka na kumaliza chuki. Kiliwazo hiki kinalazimu kulingana na hali ya mwanamume aliyetoa talaka: tajiri kulingana na ukunjufu wa hali yake na maskini kulingana na kile alichonacho. Kiliwazo hiko kiwe ni chenye kuambatana na Sheria. Nacho ni haki iliyothibiti juu ya wale wanaowafanyia wema watalaka wao na kujifanyia wema wao wenyewe kwa kumtii Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net