Al-Baqara 2:242
البقرةكَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Namna hivi ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu. [242]
[242] Mwenyezi Mungu anakubainishieni hukumu zake, na neema zake, na Aya zake, kwa mfano wa bayana hizi na Sharia hizi zilizo wazi zenye kuleta maslaha, ili mpate kuzingatia na mpate kutenda yaliyo kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfano wa maelezo hayo yaliyo wazi, katika hukumu za watoto na wanawake, Anawabainishia Allah Mtukufu mafunzo ya aya Zake na hukumu Zake kuhusu kila mnachokihitajia katika maisha yenu ya ulimwengu na marejeo yenu ya Akhera, ili mzitie akilini mzitumie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net