Al-Baqara 2:244
البقرةوَقَـٰتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Na piganeni vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Msikizi na Mjuzi. [244]
[244] Mlivyo jua kuwa hamwezi kuyaepuka mauti kwa kuyakimbia, basi piganeni Jihadi, na zitumieni nafsi zenu kwa kulitukuza Neno la Mwenyezi Mungu, na kuweni na yakini kuwa Mwenyezi Mungu anayasikia wanayo yasema woga na wanaafiki wanao kimbia, na wayasemayo Mujaahidina wanao pigana, na anayajua anayo dhamiria kila mtu katika nafsi yake. Na kwa lilio kheri atamlipa kheri, na kwa shari atamlipa shari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na piganeni nao, enyi Waislamu, hao makafiri ili kuinusuru Dini ya Allah Mtukufu, na mjue kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu na ni Mwenye kuzijua nia zenu na vitendo vyenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net