Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 245

Al-Baqara 2:245

البقرة

مَّن ذَا ٱلَّذِى يُقْرِضُ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَـٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَٱللَّهُ يَقْبِضُ وَيَبْصُۜطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Maana

Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema; ili amzidishie mizidisho mingi. Na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na kwake Yeye mtarejeshwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea. [245]

[245] Na Jihadi kwa Njia ya Mwenyezi inhaitaji mali, basi toeni mali yenu. Mtu gani huyo ambaye hatoi mali yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa radhi ya nafsi yake, na hali Mwenyezi Mungu ameahidi kuwa atamrejeshea mara nyingi sana zaidi? Na riziki zote zimo katika mkono wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye humkunjia amtakaye na akamkunjulia amtakaye kwa yaliyo na maslaha yenu. Marejeo ni kwake Yeye, naye atakulipeni kwa mujibu mlivyo toa. Na ilivyo kuwa riziki zote ni kwa fadhila ya Mwenyezi na Yeye ndiye mwenye kutoa na mwenye kunyima basi ameitwa yule mwenye kutoa kuwa ni kama mkopeshaji ili kuhimiza na kupendekeza kutoa, na kutilia mkazo kuwa malipo ni mara nyingi sana duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni yupi ambaye atatoa katika njia ya Allah Mtukufu, kutoa kuliko kuzuri kwa kutarajia malipo, Allah Mtukufu Apate kumuongezea nyongeza nyingi zisizohesabika za thawabu na malipo mema? Hakika Allah Mtukufu Anazuia na Anatoa. Kwa hivyo, toeni wala msijali, kwani Yeye Ndiye Mruzuku, Anambana Anayemtaka, miongoni mwa waja Wake, katika riziki na Anaikunjua, hiyo riziki, kwa wengine. Ana hekima kubwa katika hayo. Na Kwake Yeye Peke Yake mtarudi baada ya kufa, na hapo Atawalipa kwa vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net