Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 234

Al-Baqara 2:234

البقرة

وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Maana

Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanaacha wake, hawa wake wazizuie nafsi zao miezi minne na siku kumi. Na wanapotimiza muda wao (wa eda), basi hakuna ubaya wowote juu yao katika yale wanayojifanyia kwa wema. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya kwao kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. [234]

[234] Miongoni mwenu enyi wanaume, akitokea aliye kufa akaacha mke asiye na mimba, basi mwanamke yampasa akae eda, yaani asiolewe, muda wa miezi mine ya kuandama na siku kumi mchana na usiku, ili kuhakikisha kiliomo tumboni, kama ana mimba au la. Ukisha muda huu, enyi wazee, hapana ubaya kwenu mkiwaachilia kuleta mtu wa hishima kuja mposa. Haifai nyinyi kuwazuilia hayo, na haijuzu kwao kufanya mambo yanayo kataliwa na Sharia, kwani Mwenyezi Mungu anajua vyema siri zenu na anavijua vitendo vyenu, na atakuhisabuni kwa myatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanaofariki kati yenu wakawaacha wake zao baada ya kufa kwao, italazimu wakae eda muda wa miezi minne na siku kumi, wasitoke majumbani mwao, wasijipambe wala wasiolewe. Na pindi muda huo uliotajwa uishapo, si dhambi kwenu, enyi mawalii wa wanawake, kwa yale watakayo kujifanyia nafsi zao, ya kutoka, kujipamba na kuolewa kwa njia iliyowekwa na Sheria. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kutakasika na kila sifa mbaya, ni Mtambuzi wa vitendo vyenu vya wazi na viliyofichika, na Atawalipa kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net