Al-Baqara 2:211
البقرةسَلْ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ كَمْ ءَاتَيْنَـٰهُم مِّنْ ءَايَةٍۭ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ
Waulize Wana wa Israili: 'Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi?' Na anayezibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi? Na anaye zibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. [211]
[211] Waulize Wana wa Israili tumewaletea dalili ngapi za kukata za kuthibitisha ukweli wa Mtume! Na hayo ni neema ya kutaka kuwaongoa wamwendee Mwenyezi Mungu. Lakini wapi! Walizikataa hizo dalili na wakashikilia kuzikanusha hadi ya kuyageuza makusudio yake. Baada ya kuwa hizo dalili ni kwa ajili ya uwongofu zikawa kwa ukafiri wao ni sababu ya kuwazidisha upotovu na kutenda dhambi. Na mwenye kugeuza neema ya Mwenyezi Mungu kwa namna hii basi huyo anastahiki adhabu, na Mwenyezi Mungu hakika ni mkali wa kuadhibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waulize, ewe Mtume, Wana wa Isrãîl wanaokufanyia ukaidi, «Ni aya ngapi zilizo wazi tulizowapa katika vitabu vyao zinazowaongoza wao njia ya haki, wakazikanusha,wakazipa nyongo na wakazipotosha kwa kuzitoa kwenye malengo yake.» Na atakayebadilisha neema ya Allah Mtukufu, nayo ni dini Yake, na akaikanusha baada ya kuijua na hoja yake kumsimamia, basi Allah Mtukufu ni Mkali wa mateso kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net