Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 210

Al-Baqara 2:210

البقرة

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأْتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِى ظُلَلٍ مِّنَ ٱلْغَمَامِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَقُضِىَ ٱلْأَمْرُ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ

Maana

Je, wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na hukumu iwe imekwishatolewa? Na kwa Mwenyezi Mungu ndiyo hurejeshwa mambo yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na hukumu iwe imekwisha tolewa? Na kwa Mwenyezi Mungu ndio hurejeshwa mashauri yote. [210]

[210] Je, hao wanao ukataa Uislamu wanangojea mpaka wamwone Mwenyezi Mungu Mtukufu na Malaika jahara katika mawingu na hukumu ya kuwakatisha tamaa zao imekwisha pitishwa? Kwani hakika mambo yote yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Yeye huyasarifu atakavyo, na hukumu yake imekwisha tolewa, na hapana shaka yoyote itatekelezwa tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawangojei hawa wakaidi wenye kukanusha, baada ya kusimama dalili wazi, isipokuwa Awajie Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kushinda, kwa namna inayolingana na Yeye, Aliyetakasika na kila sifa mbaya, katika vivuli vya Mawingu Siku ya Kiyama ili Aamue baina yao kwa hukumu adilifu, na waje Malaika. Wakati huo, Atahukumu Allah Mtukufu, kati yao, hukumu Yake. Na kwake Yeye Peke Yake hurudishwa mambo yote ya viumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net