Al-Baqara 2:209
البقرةفَإِن زَلَلْتُم مِّنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْكُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na mkiteleza baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi, basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikiwa mkateleza baada ya kukufikieni hoja zilizo wazi, basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [209]
[209] Mkigeuka mkaiacha Njia hii mliyo itiwa muifuate nyote baada ya kudhihiri hoja za kukata kuwa ndiyo Njia ya Haki, basi jueni mtapatilizwa kwa kugeuka huko, kwani Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye nguvu, humuadhibu mwenye kuiacha Njia yake, na Mwenye hikima anaye pima kadiri ya adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iwapo mtapondoka kwenye njia ya haki, baada ya kujiliwa na hoja wazi wazi za Qur’ani na Suna, basi jueni kwamba Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake, hakuna chochote kilicho nje ya mamlaka Yake, ni Mwingi wa hekima kwenye amri Zake na Makatazo yake, Anaweka kila kitu pahali pake palinganapo nacho.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net