Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 212

Al-Baqara 2:212

البقرة

زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ فَوْقَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ وَٱللَّهُ يَرْزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ

Maana

Waliokufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na wanawafanyia masihara wale walioamini. Na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio kufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na wanawafanyia maskhara walio amini. Na wenye kuchamngu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu. [212]

[212] Na sababu ya kupotoka na kukufuru ni kuitaka dunia. Wale walio kufuru wamepambiwa matamanio ya maisha ya kidunia wakawa wanawakejeli wale walio amini kwa kushughulikia kwao maisha ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu atawaweka walio amini pahala pa juu kabisa kuliko wao katika Akhera. Ama kuwa hawa makafiri wana mali zaidi na mapambo ya kidunia hakuonyeshi ubora wao, kwani riziki ya Mwenyezi Mungu haipimwi kwa mujibu wa kuamini na kukufuru, bali inakwenda kama apendavyo Yeye mwenyewe. Wapo watu huzidishiwa hiyo riziki kwa "Istidraaji" kumpururia kamba tu, na wapo wanao nyimwa neema za dunia kama ni mtihani, majaribio.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale walioukanusha upweke wa Allah Mtukufu wamepambiwa maisha ya dunia na vilivyomo humo vya matamanio na vilivyo tamu, na huku wao wanawafanyia shere Waumini. Na hawa wanaomcha Mola wao watakuwa juu ya Makafiri wote Siku ya Kiyama, ambapo Allah Mtukufu Atawatia katika Pepo ya daraja za juu na Atawateremsha Makafiri ndani ya mashimo ya Moto ya chini. Allah Mtukufu Anamruzuku Amtakaye, katika viumbe vyake, bila ya hesabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net