Al-Baqara 2:206
البقرةوَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتْهُ ٱلْعِزَّةُ بِٱلْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُۥ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
Na akiambiwa, “Mche Mwenyezi Mungu,” hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo kinachomtosha ni Jahannam. Napo hakika ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa mapumziko. [206]
[206] Akinasihiwa amwogope Mwenyezi Mungu huzidi kupanda mori wake na akadhani kuwa hivyo unamvunjia cheo chake, akazidi kupanda madhambi na kuzidi kumchafua na kumwongeza inadi. Mtu huyo hatoshelezeki mpaka aingie Jahannam, na hayo ni makao maovu mno.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na anaponasihiwa mnafiki huyo mharibifu na akaambiwa, «Mche Allah Mtukufu,ujihadhari na adhabu Yake na ukomeke na kuleta uharibifu katika ardhi,» huwa hakubali nasaha. Bali kile kiburi chake na mori wa kijinga humfanya kutenda maovu zaidi. Basi adhabu yenye kumtosheleza yeye ni Jahanamu. Na hakika hilo ni godoro baya kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net