Al-Baqara 2:205
البقرةوَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ ٱلْحَرْثَ وَٱلنَّسْلَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلْفَسَادَ
Na akishageuka akaenda, anazunguka katika ardhi ili afanye humo uharibifu na kuangamiza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi. [205]
[205] Na pindi wakitawalishwa madaraka yoyote haiwi juhudi yao kuleta maslaha, bali ni kuleta ufisadi na kuteketeza mimea, kukata miti na kuuwa wanyama na binaadamu. Na Mwenyezi hawapendi watu kama hawa, kwani Mwenyezi Mtukufu hapendi uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na anapoondoka kutoka kwako, ewe Mtume, hufanya bidii na akachangamka katika ardhi ili alete uharibifu humo na kuharibu mazao ya watu na kuua wanyama wao. Na Allah Mtukufu Hapendi uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net