Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 204

Al-Baqara 2:204

البقرة

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُۥ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَيُشْهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِى قَلْبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلْخِصَامِ

Maana

Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukupendeza; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyo katika moyo wake, na hali yeye ndiye mgomvi mkubwa mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu. [204]

[204] Ilivyo kuwa kumcha Mwenyezi Mungu ndio msingi, basi khasara ni ya wale watu ambao dhamiri walio nayo nyoyoni mwao ni mbali na maneno yanayo tamkwa na ndimi zao. Wamepewa utamu wa kupanga maneno, hukufurahisha kauli yao katika kujivutia manufaa ya maisha ya kidunia, na kuunga mkono kwa wayasemayo humsingizia Mwenyezi Mungu kuwa anashuhudia kuwa wayasemayo yanatoka nyoyoni mwao. Kumbe wao kwa hakika ndio wakubwa wa ukhasama na ukhabithi kwako wewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na baadhi ya watu miongoni mwa wanafiki yanakuvutia, ewe Mtume, maneno yake yaliyo fasaha ambayo kwayo anataka fungu la hadhi za duniani, si za Akhera, na anaapa huku akimshuhudisha Allah Mtukufu yaliyo moyoni mwake ya kuupenda Uislamu, hali ya kuwa yeye ana uadui na utesi mkubwa juu ya Uislamu na Waislamu. Huo ni upeo wa kujifanya ujasiri juu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net