Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 203

Al-Baqara 2:203

البقرة

وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ فِىٓ أَيَّامٍ مَّعْدُودَٰتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِى يَوْمَيْنِ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ ٱتَّقَىٰ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Maana

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazohisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka (akarejea) katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake. Na mwenye kukawia, pia hakuna dhambi juu yake, kwa mwenye kumcha Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake. [203]

[203] Na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa Takbiri na vinginevyo katika siku maalumu, nazo ni siku za kutupa mawe hapo Mina, nazo ni taarikh 11 na 12 na 13. Na si lazima kwa Haji kukaa siku tatu hizi Mina akitupa mawe, bali anaweza kufupiza siku mbili, kwani msimamo wa kheri ni kuchamngu, si idadi. Na daima mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa kwake Yeye mtakusanywa na muulizwe mliyo yatenda. Hayo mawe ni changarawe hutupwa mwahala maalumu katika Mina katika siku ya kuchinja (Idd) na siku tatu zifwatiazo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mtajeni Allah Mtukufu kwa kuleta Tasbihi na Takbiri, katika siku chache, nazo ni siku za Tashrîq: siku ya kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu za mwezi wa Mfungotatu.Atakaye kufanya haraka kuondoka Mina kabla ya kuchwa jua la siku ya kumi na mbili, baada ya kurusha vijiwe, hana makosa. Na yule atakaye kuchelewa kwa kulala Mina kungojea mpaka arushe vijiwe siku ya kumi na tatu, pia hana makosa, kwa aliyemcha Allah Mtukufu katika Hija yake. Na kuchelewa ni bora zaidi, maana huko ni kujiongezea mapato katika ibada na kufuata kitendo cha Nabii Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie. Na muogopeni Allah Mtukufu, enyi Waislamu, na mumweke mbele katika amali zenu zote; na mjue kwamba nyinyi kwake Yeye Peke Yake mtakusanywa baada ya kufa kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net