Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتْهُ ٱلْعِزَّةُ بِٱلْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُۥ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ 206
(206) Na “hupandwa na mori wa kutenda madhambi.” Kwa hivyo anajumuisha kati ya kufanya maasia na kiburi kwa wanaomshauri. “Basi huyo kinachomtosha ni Jahannam,” ambayo ndio makazi ya wafanyao maasia na wanaotakabari. “Napo hakika ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.” Yani pahali pa kukaa na maskani, yenye adhabu ya daima, na huzuni isiyoisha, na kukata tamaa kwenye kuendelea. Hawatapunguziwa adhabu, wala hawatarajii malipo mazuri. Haya ni malipo ya makosa yao na matendo yao. Basi Mwenyezi Mungu atuepushe na hali zao.