Al-Baqara 2:207
البقرةوَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشْرِى نَفْسَهُ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ رَءُوفٌۢ بِٱلْعِبَادِ
Na katika watu, kuna yule anayeiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. [207]
[207] Ni farka kubwa baina ya wanaafiki hawa na Waumini wa kweli ambao watayari kuuza nafsi zao kwa sababu ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kulitukuza Neno la Haki. Hawa ni kinyume na wale wa kwanza. Hawa wakitawalishwa madaraka kuendesha mambo ya watu inakuwa ni katika upole wa Mwenyezi Mungu kuwafanyia waja wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu huwarehemu hao waja wema kwa kuwatawalisha watu wema ili awalinde na wenye shari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na baadhi ya watu huziuza nafsi zao kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu, kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kujilazimisha kumtii. Na Allah Mtukufu ni Mpole kwa waja, Anawarehemu waja wake Waumini rehema kunjufu, katika ulimwengu wao na Akhera yao, na kuwalipa malipo mazuri zaidi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net