Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 159

Al-Baqara 2:159

البقرة

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَآ أَنزَلْنَا مِنَ ٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلْهُدَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا بَيَّنَّـٰهُ لِلنَّاسِ فِى ٱلْكِتَـٰبِ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ يَلْعَنُهُمُ ٱللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ ٱللَّـٰعِنُونَ

Maana

Hakika, wale wanaoficha yale tuliyoyateremsha, nazo ni hoja zilizo wazi na uongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani. [159]

[159] Hao wanao kukatalieni Dini yenu wako makundi mawili: kundi moja ni katika Watu wa Kitabu wanao ijua Kweli, lakini wanaificha kwa kujua na kwa inda. Na kundi jengine ni la washirikina ambao nyoyo zao ni pofu, kwa hivyo hawaioni Kweli, na badala ya Mwenyezi Mungu Mmoja wakawa wanaabudu miungu myengineo. Basi Watu wa Kitabu walio jua ushahidi wa ukweli wako wanajua haki ya Dini yako, lakini kisha wanazificha hizo dalili ili watu wasijue. Mwenyezi Mungu atawapatiliza ghadhabu yake, na atawaepusha rehema yake, na kila wanao omba katika Malaika, na Wanaadamu na Majini watawaapiza wasipate rehema ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao wanazificha aya zilizo waziwazi, zijulishazo utume wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, nao ni wanavyuoni wa Kiyahudi na wajuzi wa Kinaswara na wengineo, miongoni mwa wafichao yaliyoteremshwa na Allah Mtukufu, baada ya sisi kuyadhihirisha kwa watu katika Taurati na Injili, hao Allah Mtukufu Atawafukuza kutoka kwenye rehema Yake, na viumbe wote watawaapiza laana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net