Al-Baqara 2:160
البقرةإِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ وَأَصْلَحُوا۟ وَبَيَّنُوا۟ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Isipokuwa wale waliotubu, wakatengeneza na wakabainisha. Basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. [160]
[160] Wala hapana atakaye vuka na laana hiyo katika wao ila aliye tubu na akatenda mema kwa kuacha kuficha Haki, akayadhihirisha aliyo kuwa akiyaficha katika sifa za Mtume na Uislamu. Mwenyezi Mungu atakubali toba yake na atamfutia dhambi zake, kwani Yeye ndiye anaye kubali toba ya waja wake kwa huruma na rehema yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Isipokuwa wale waliorudi hali ya kutubia makosa yao, wakarekebisha waliyoyaharibu na wakayabainisha waliyoyaficha. Hao nitazikubali toba zao na nitawalipa kwa kuwasamehe. Na mimi ni Mwenye kukubali mno toba ya mwenye kutubia kati ya waja Wangu na ni Mwenye huruma kwao kwa kuwapa taufiki ya kutubia na kukubali toba kutoka kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net