Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ وَأَصْلَحُوا۟ وَبَيَّنُوا۟ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ 160
“Isipokuwa wale waliotubu,” yani waliyaacha madhambi yao na wakajuta na kuwachana nayo kabisa, na wakaazimia kutorejea. “Wakatengeneza” yale waliyoharibika katika matendo yao. Na haitoshi kuacha ubaya tu mpaka kupatikane kufanya mema. Na hilo pia halitoshi kwa mwenye kuficha mpaka abainishe yale aliyoyaficha, na aonyeshe kinyume cha aliyoyaficha. Basi huyu, Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake, kwa sababu toba ya Mwenyezi Mungu haizuiliwi. Basi, atakayefanya sababu ya toba, Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake, kwa sababu yeye ndiye, “Mwenye kupokea toba.” Yani kuwarudia waja wake kwa kuwasamehe na kuwachilia baada ya dhambi wakitubu, wanapotubu. Na kwa wema na neema baada ya kuzuia wakirejea, “Mwenye kurehemu.” Ambaye anasifika kwa rehema kubwa ambayo inaenea kila kitu. Na katika rehema yake ni kuwa aliwawezesha kutubu na kurudi kwake, kwa hivyo wakatubu na wakarudi kwake. Kisha akawarehemu kwa kukubali hayo kutoka kwao, kwa upole na ukarimu. Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kutubia dhambi.