Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 152

Al-Baqara 2:152

البقرة

فَٱذْكُرُونِىٓ أَذْكُرْكُمْ وَٱشْكُرُوا۟ لِى وَلَا تَكْفُرُونِ

Maana

Basi nitajeni, nitakutajeni. Na nishukuruni, wala msinikufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru. [152]

[152] Basi enyi Waumini! Nikumbukeni kwa kunit'ii, na Mimi nitakukumbukeni kwa kukupeni thawabu. Na nishukuruni kwa neema nilizo kuvikeni, wala msizipinge neema hizi kwa kuyaasi yale niliyo kuamrisheni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amewaamrisha Waumini wamtaje Yeye na Akatoa ahadi kwa hilo malipo bora zaidi, nayo ni kumsifu yule anayemtaja Yeye mbele ya viumbe walioko juu. Pia Amewaamrisha Waumini wamshukuru Yeye Peke Yake kwa maneno na vitendo na wasizikanushe neema Zake juu yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net