Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَٱذْكُرُونِىٓ أَذْكُرْكُمْ وَٱشْكُرُوا۟ لِى وَلَا تَكْفُرُونِ 152
(152) “Basi nikumbukeni nitakukumbukeni.” Basi Mola Mtukufu akaamrisha kumkumbuka, na akaahidi malipo bora zaidi juu yake, ambayo ni kukumbuka kwake mwenye kumkumbuka. Kama alivyosema Mtukufu juu ya ulimi wa Mtume wake. “Mwenye kunikumbuka katika nafsi yake, basi mimi natamkumbuka katika nafsi yangu. Na mwenye kunikumbuka katika mkusanyiko, nitamkumbuka katika mkusanyiko bora kuliko wao.” Na kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko bora zaidi ni kule ambako moyo na ulimi vimekubaliana ju yake. Nako ndiko [kukumbuka] ambako kunaoleta kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda, na wingi wa malipo yake. Na kukumbuka ndiko kichwa cha shukurani. Ndio maana akaliamrisha hilo hasa, kisha baada yake akaamrisha kushukuru kwa ujumla, akasema, “na nishukuruni”. Yani kwa yale niliyokuneemesheni kwa neema hizi, na nikawaondolea kila aina ya maovu. Na kushukuru kunakuwa pia kwa moyo kwa kukiri na kutambua neema. Na kwa ulimi kwa kutaja na kusifu. Na kwa viungo kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kutekeleza amri zake na kuacha makatazo yake. Na katika kushukuru kuna kuendelea kubakia kwa neema iliyopo, na kuongezwa neema zisizokuwepo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “mkishukuru, nitakuzidishieni.” Na katika kuweka amri ya kushukuru baada ya neema za kidini kama vile elimu, utakaso wa maadili, na na kuwezeshwa katika matendo; kuna kubainisha kuwa hizo ndizo neema kubwa zaidi. Bali ndizo neema za kihakika ambazo zinadumu zinapotoweka neema zinginezo. Na kwamba inampasa mwenye kuwezeshwa elimu au tendo fulani kwamba, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo ili awazidishie katika fadhila zake na ili kujisifu kujiepushe nao. Na pia wajishughulishe na kushukuru. Na kilipokuwa kinyume cha kushukuru ni kukufuru, akasema, “wala msinikufuru.” Na kilichokusudiwa na kukufuru hapa ni kinyume cha kushukuru, nako ni kukufuru neema na kuzikanusha na kutozitekeleza. Na inawezekana kuwa maana yake ni ya jumla, kwa hivyo kukawa kukufuru kuna aina nyingi, kubwa zaidi ikiwa ni kumkufuru Mwenyezi Mungu. Kisha aina za maasia mbalimbali na jinsi zake kama shirki na kilichoko chini yake.