Al-Baqara 2:153
البقرةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَعِينُوا۟ بِٱلصَّبْرِ وَٱلصَّلَوٰةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika, Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. [153]
[153] Na tafuteni kujisaidia, enyi Waumini, katika kila linalo kupateni, kwa kusubiri na kushika Swala. Swala ndio msingi wa ibada zote. Hakika Mwenyezi Mungu kwa uwezo wake wenye nguvu yu pamoja na wanao subiri. Yeye ndiye mlinzi wao, na Yeye ndiye anaye wanusuru daima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi Waumini, takeni msaada kutoka kwa Allah Mtukufu katika mambo yenu yote, kwa kusubiri juu ya mikasa na misiba, na kuacha maasia na madhambi na kusubiri juu ya kufanya mambo ya utiifu na yale yanayomkurubisha mtu kwa Mola wake, na kwa Swala ambayo kwayo nafsi inapata utulivu na ambayo inakataza machafu na maovu. Hakika Allah Mtukufu Yuko pamoja na wenye kusubiri kwa msaada Wake, taufiki Yake na muelekezo Wake. Katika hii Aya kuna kuthibitisha kuwa Allah Mtukufu Yuko pamoja na Waumini kimahsusi, upamoja unaolazimiana na yaliyotangulia kutajwa. Ama kuwa Allah Mtukufu yuko pamoja na viumbe kijumla kunakolazimiana na elimu Yake na kuwa ujuzi Wake umezunguka kila kitu, basi upamoja huo ni wa viumbe vyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net