Al-Baqara 2:154
البقرةوَلَا تَقُولُوا۟ لِمَن يُقْتَلُ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمْوَٰتٌۢ ۚ بَلْ أَحْيَآءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ
Wala msiseme kuwa wale waliouwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti. Bali hao ni hai. Lakini nyinyi hamtambui.[1]
[1] Inajulikana kuwa kipenzi hakiachwi na wenye akili timamu, isipokuwa kwa ajili ya kipenzi kilicho juu zaidi na kikubwa kukiliko. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuuawa katika njia yake akipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi; na dini yake iwe iliyo dhahiri zaidi. Basi yeye kwa hakika hajakosa uhai alioupenda, bali (alipouawa) alipata uhai mkubwa na kamili zaidi kuliko mnavyofikiria nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui. [154]
[154] Na subira haipelekei ila kwenye kheri na kufanikiwa kote kuwili, duniani na Akhera. Basi msikae nyuma mkaacha kwenda kupigana Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Wala msiogope kufa katika Jihadi, kwani mwenye kufa katika Jihadi huyo si maiti, hakufa, bali yuhai maisha ya juu kabisa, ijapo kuwa hawa tunao waona wahai hawatambui hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wala msiseme, enyi Waumini, kuhusu wale wanaouawa hali ya kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, kuwa wao wamekufa. Bali wao wako hai, uhai maalumu unaowahusu wao, ndani ya Makaburi yao. Wala hakuna anayejua yako vipi maisha hayo isipokuwa Allah Mtukufu, lakini nyinyi hamuyahisi maisha hayo. Katika haya, pana ushahidi kwamba kuna neema za kaburini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net