Al-Baqara 2:155
البقرةوَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَىْءٍ مِّنَ ٱلْخَوْفِ وَٱلْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ ٱلْأَمْوَٰلِ وَٱلْأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِ ۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Hapana shaka, tutakujaribuni kwa chembe ya hofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na mazao. Na wabashirie wanaosubiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, [155]
[155] Subira ni ngao na silaha ya Muumini ambayo kwayo hushindia kila shida na mashaka. Na nyinyi zitakuja kupateni shida nyingi. Tutakujaribuni na kukufanyieni mitihani kwa vitisho vya maadui, kwa njaa, na uchache wa vifaa, na kupungukiwa mali, na watu kufa, na kupotea mazao. Na hapana la kukulindeni katika mtihani huu mkali ila Subira. Basi Ewe Nabii! Wape bishara nzuri wanao subiri kwa moyo na ulimi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tutawapa, tena tutawapa, mtihani wa kitu hafifu cha hali ya kuogopa, njaa, upungufu wa mali, iwe ni uzito kuyapata au yaondoke, upungufu wa watu: kwa kufa au kufa-shahidi-. katika njia ya Allah Mtukufu, na kwa upungufu wa matunda ya mitende na mizabibu na nafaka: kwa kupungua mazao yake au kuharibika kwake. Wape, ewe Nabii, habari njema, wale wenye subira juu ya haya na mfano wake, kwa yale yatakayowafurahisha na kuwapendeza ya mwisho mwema duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net