Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 151

Al-Baqara 2:151

البقرة

كَمَآ أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا۟ تَعْلَمُونَ

Maana

Kama tulivyomtuma Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anawasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima, na anawafundisha ambayo hamkuwa mnayajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana na nyinyi, anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hikima na kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui. [151]

[151] Na hivi kukuelekezeni kwenye Msikiti Mtakatifu na kwa kuwa tumekutumieni Mtume aliye tokana nanyi, akikusomeeni Aya ni katika kukutimizieni neema yetu, kama tulivyo kutimizieni ile neema - nayo ni Qur'ani - na akusafishieni nafsi zenu zitoke uchafu wa ushirikina na tabia na ada mbovu mbovu, na anakusemezeni kwa njia ya kukufunzeni maarifa ya Qur'ani na ilimu zenye nafuu, na kukufunzeni mambo ambayo mlikuwa hamyajui. Kwani mlikuwa katika ujinga na upotovu ulio mpofu wa kijahilia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kama Tulivyowaneemesha kwa kuelekea Alkaba, Tumewaletea mjumbe anayetokana na nyinyi, anawasomea aya zibainishazo haki kuitenga na batili, kuwasafisha na uchafu wa ushirikina na tabia mbaya, kuwafundisha Kitabu, Sunna na hukumu za Sheria na kuwafundisha habari za Mitume na visa vya ummah waliopita, mambo ambayo mlikuwa hamyajui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net