Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 150

Al-Baqara 2:150

البقرة

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا۟ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَٱخْشَوْنِى وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِى عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Maana

Na kokote uendako, uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo, zielekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi, msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi. Na ili niwatimizie neema yangu, na ili mpate kuongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka. [150]

[150] Jilazimishe kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu katika mambo ya kuelekea Kibla, na kuwa na pupa nayo wewe na umma wako. Na uelekeze uso wako uelekee upande wa Msikiti Mtakatifu popote wendapo katika safari zako. Na elekeeni huko popote mtapo kuwapo pande zote za dunia, mkiwa mko safarini au mpo mjini, ili ukatike ule ushindani wa hoja za hao walio khalifu na wanao jadiliana nanyi ikiwa hamkufuata amri hii ya kugeuza Kibla. Mayahudi watasema: Vipi Muhammad anapo sali anaelekea Beitul Muqaddas, na Nabii alielezwa katika vitabu vyetu ni kuwa moja katika sifa zake anaelekea Alkaaba? Na washirikina wa Kiarabu watasema: Vipi anadai kuwa mila yake ni mila ya Ibrahim, naye hafuati Kibla chake? Juu ya vyote hakika hao walio dhulumu walio potoka wakaiacha Haki kutoka pande zote mbili hawatoacha majadiliano yao na upotovu wao, bali watasema: Hakugeuka kuelekea Alkaaba ila kuwa anafuata ile ile dini ya kishirikina ya kaumu yake, na kuupenda ule mji wake. Basi nyinyi msiwabali hao, kwani uchochezi wao hauto kudhuruni. Nanyi niogopeni Mimi, msiikhalifu amri yangu. Kwa amri hii tumetaka kuitimiza neema juu yenu, na Kibla hichi tulicho kuelekezeni ndicho kipelekee kuthibiti kwenu katika uwongofu na kupata tawfiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mahali popote uendapo, ewe Nabii, elekea Msikiti wa Ḥaram. Na popote mnapokuwa, enyi Waislamu, katika nchi yoyote miongoni mwa nchi za ardhi, elekezeni nyuso zenu upande wa Msikiti wa Ḥaram, ili watu wapinzani wasiwe na hoja yoyote kwenu kwa njia ya ugomvi na mjadala, baada ya kuelekea huko, isipokuwa wale madhalimu na wenye ukaidi kati yao. Hao watabakia kwenye mjadala wao. Basi, msiwaogope wao, niogopeni Mimi kwa kufuata amri Yangu na kujiepusha na katazo Langu na ili nikamilishe neema Zangu kwenu kuwachagulia sheria zilizokamilika zaidi, na ili mpate kuongoka kufuata haki na usawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net