Al-Baqara 2:149
البقرةوَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُۥ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ
Na kokote uendako, uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika mbali na mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. [149]
[149] Basi katika Swala zako popote pale ulipo uelekee Msikiti Mtakatifu, ukiwa upo mjini au umo safarini, popote wendapo. Na hakika haya bila ya shaka ndiyo ya Haki yanayo wafikiana na hikima ya Mola wako Mlezi aliye pamoja nawe. Basi wewe na umma wako yatamanini haya. Kwani Mwenyezi Mungu atakulipeni malipo mema kabisa. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi wala hapana katika vitendo vyenu vilivyo fichikana naye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na popote unapoenda, ewe Nabii, ukiwa msafiri na ukataka kuswali, elekeza uso wako upande wa Msikiti wa Ḥaram. Kuelekea kwako huko ndio haki iliyothibiti kutoka kwa Mola wako. Na Allah Mtukufu hakuwa ni Mwenye kughafilika juu ya yale mnayoyatenda na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net