Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 148

Al-Baqara 2:148

البقرة

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَٱسْتَبِقُوا۟ ٱلْخَيْرَٰتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا۟ يَأْتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Na kila mmoja anao mwelekeo anaoelekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kila mmoja anao upande anao elekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo Mwenyezi Mungu atakuleteni nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [148]

[148] Hakika Kibla hicho tulicho kuelekeza ndicho Kibla chako na Kibla cha Umma wako. Na hali kadhaalika kila umma una kibla chake unako elekea katika swala yao kwa mujibu wa sharia zilizo kwisha pita. Wala katika haya hapana kupikuana kwa ubora, na ama kupikuana kwa ubora ni kwa kutenda vitendo vya ut'iifu na a'mali za kheri. Basi kimbilieni kwenye kheri na mshindane kwa hayo. Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwa hayo, kwani Yeye atakukusanyeni nyote Siku ya Kiyama kutoka kokote mtapo kuwako. Wala hatamchopoka hata mmoja. Kila kitu kimo mkononi mwake, na katika hivyo ni amana, kuhuisha, kufufua na kukusanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila ummah, miongoni mwa ummah wa kila aina, una kibla chake anachokielekea kila mmoja katika wao kwenye swala yake. Basi kimbilieni, enyi Waumini, hali ya kushindana katika kutenda vitendo vyema ambavyo Ameviwajibisha kwenu Allah Mtukufu katika Dini ya Kiislamu. Allah Mtukufu Atawakusanya nyote Siku ya Kiyama kutoka popote mtakapokuwa. Hakika Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net