Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 147

Al-Baqara 2:147

البقرة

ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ

Maana

Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. [147]

[147] Na hakika Haki ni anayo kutolea Mwenyezi Mungu Mtukufu sio wanayo kupotoshelea watu wa Kitabu. Basi kuweni na yakini nayo, msiwe watu wenye kutia shaka shaka na kubabaika. Na katika hiyo Haki ni hii amri ya Kibla, basi endeleeni nayo wala msiwabali (musiwajali) wapinzani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yale yaliyoteremshwa kwako, ewe Nabii, ndiyo haki kutoka kwa Mola wako. Kwa hivyo, usiwe ni kati ya wale wanaoyatilia shaka. Maneno haya, ingawa anambiwa Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, yanaelekezwa kwa ummah wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net