Al-Baqara 2:146
البقرةٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْرِفُونَهُۥ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَآءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ ٱلْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Wale tuliowapa Kitabu, wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao. Na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao; na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua. [146]
[146] Na hakika Watu wa Kitabu wanajua kuwa huku kugeuza Kibla ni jambo la haki, na wanakutambua kuwa wewe ndiye Nabii aliye sifiwa katika vitabu vyao, na miongoni mwa sifa hizo kuwa atasali kuelekea Alkaaba. Na kujua kwao Unabii wako na kukijua Kibla chako ni sawa sawa wanavyo wajua watoto wao kwa uwazi kabisa. Lakini baadhi yao wanaificha kweli hii juu ya kuwa wanajua, kwa kufuata pumbao na chuki zao za upotovu kuwania mila zao kwa ajili ya kulinda madaraka yao, na wanatafuta hila za kukupotoeni nyie.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale Tuliowapa Taurati na Injili miongoni mwa wanavyuoni wa Kiyahudi na wajuzi wa Kinaswara wanajua ya kwamba Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni mjumbe wa Allah Mtukufu, kwa sifa zake zilizotajwa katika vitabu vyao, kama vile wanavyowajuwa wana wao. Na hakika kuna kundi kati yao wanaificha haki na wao wanaujua ukweli wake na kuwa sifa zake zimethibiti.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net