Al-Baqara 2:125
البقرةوَإِذْ جَعَلْنَا ٱلْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَٱتَّخِذُوا۟ مِن مَّقَامِ إِبْرَٰهِـۧمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَآ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِىَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلْعَـٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ
Na kumbukeni tulipoifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahali pa kukusanyikia watu na pahali pa amani. Na alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga huko kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu. [125]
[125] Na kadhaalika kumbukeni hadithi ya Ibrahim na mwanawe Ismail walipo ijenga ile Nyumba Takatifu ya Makka, Alkaaba. Katika kisa hichi pana funzo linalo fika mbali kwa mwenye moyo wa kuzingatia. Basi kumbukeni tulipo ifanya Nyumba hii ni pahala wanapo kwenda viumbe kutoka kila pahala duniani na kukusanyika. Na tukaifanya kuwa ni pahala pa usalama na amani kwa kila mwenye kutaka hifadhi. Na pia tulivyo amrisha kuwa pahala alipo kuwa akisimama Ibrahim kuijenga hiyo Nyumba pafanywe ni msala, yaani pahala pa kusalia. Na tukaagana na Ibrahim na Ismail waihifadhi Nyumba hiyo isipate kitu ambacho hakistahiki na utakatifu wake, na waitayarishe kwa matayarisho yanayo silihi kwa wanao kusanyika huko, wale wanao kwenda kut'ufu, na wanao kaa kwa ibada ya ii'tikafu, na wanao sali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Nabii, wakati tulipoifanya Alkaba ni marejeo ya watu; wanakuja kuikusudia, kisha wanarudi makwao kwa watu wao, kisha wanairudia tena, ni makusanyiko yao katika Hija, Umra, kutufu na kuswali, na pia ni amani kwao: hakuna adui anayewashambulia wakiwa hapo na tukasema, “Pafanyeni hapo Maqãm Ibrahîm ni mahali pa kuswali. Maqãm Ibrahîm ni jiwe ambalo Ibrãhîm alisimama juu yake alipokuwa akijenga Alkaba. Na tulimletea Wahyi Ibrãhîm na mtoto wake Ismã’îl kwa kuwaambia, “Isafisheni Nyumba Yangu na kila najisi na uchafu kwa ajili ya wenye kuabudu kwa kutufu pembizoni mwa Alkaba au kuketi Itikafu (I’tikãf) Msikitini na kuswali hapo.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net