Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 126

Al-Baqara 2:126

البقرة

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا ءَامِنًا وَٱرْزُقْ أَهْلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنْ ءَامَنَ مِنْهُم بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Na aliposema Ibrahim: Ewe Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahali pabaya mno pa kurejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahala pabaya mno pa kurejea. [126]

[126] Na kumbukeni Ibrahim alipo mwomba Mola wake Mlezi ajaalie mji utakao kuwapo hapo kwenye nyumba ya Alkaaba uwe mji wa amani, na awaruzuku matunda ya ardhi na kheri zake watu wake watao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho. Mwenyezi Mungu alimjibu kuwa hatamnyima riziki hata kafiri muda wa uhai wake mfupi, kisha Siku ya Kiyama atakwenda ingia katika adhabu ya Jahannam, na mwisho wa watu hao ni muovu mno.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Nabii, wakati Aliposema Ibrãhîm akiwa katika maombi, “Ewe Mola wangu! ijaalie Makkah ni mji wenye amani usiokuwa na kitisho, uwaruzuku watu wake aina ya matunda na uwahusu kwa riziki hii wanaomuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho.” Allah Mtukufu Alisema, “Na mwenye kukufuru katika wao nitamruzuku ulimwenguni na kumstarehesha starehe chache, kisha nitamlazimisha kwa nguvu kwenda Motoni. Ubaya wa marejeo na makao ni mwisho huu.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net