Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 124

Al-Baqara 2:124

البقرة

وَإِذِ ٱبْتَلَىٰٓ إِبْرَٰهِـۧمَ رَبُّهُۥ بِكَلِمَـٰتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّى جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِى ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na Mola wake Mlezi alipomjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza. Akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika kizazi changu pia? Akasema: Agano langu halitawafikia wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. [124]

[124] Na kumbukeni pale Mwenyezi Mungu alipo mjaribu babu yenu Ibrahim kwa kumtwisha amri fulani. Naye Ibrahim alizitimiza hizo amri vilivyo. Mwenyezi Mungu akamwambia: Mimi nataka kukufanya wewe uwe Imamu, yaani Mwongozi, wa watu, nao wawe wakikufuata wakishika nyayo zako. Ibrahim akamtaka Mola awajaalie katika vizazi vyake wawe pia Maimamu kama yeye. Mwenyezi Mungu akamjibu kuwa haya hawatayapata wanao dhulumu, na hivyo kaashiria kuwa mnamo dhuriya za Ibrahim watatokea walio wema na walio wabaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Nabii, wakati Allah Mtukufu Alipomfanyia mtihani Ibrãhîm kwa amri Alizomkalifisha nazo, akazitekeleza na kusimama nazo kwa njia nzuri. Allah Mtukufu Akamwambia, “Mimi nimekufanya wewe ni kiigizo kwa watu.” Ibrãhîm akasema, “Ewe Mola wajaalie baadhi ya watu wa kizazi chake ni viongozi kwa ukarimu wako.” Allah Mtukufu Akamjibu kwamba madhalimu hawatapata uongozi wa kidini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net