Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 123

Al-Baqara 2:123

البقرة

وَٱتَّقُوا۟ يَوْمًا لَّا تَجْزِى نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْـًٔا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَـٰعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ

Maana

Na icheni siku ambayo hatamfaa mtu mwenziwe kwa lolote, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo, wala maombezi hayatamfaa, wala hawatanusuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na iogopeni siku ambayo hatamfaa mtu mwenziwe kwa lolote, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo, wala maombezi hayatamfaa, wala hawatanusuriwa. [123]

[123] Na iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu katika siku ambayo hapana mtu ataye weza kumtetea mwenziwe kwa lolote, wala fidia haitakubaliwa, wala maombezi hayatafaa kitu, wala makafiri hawatapata mtu wa kuwanusuru na Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ogopeni vitisho vya Siku ya Hesabu. Kwani hapo, hakuna nafsi itakayoifaa kitu chochote nafsi nyingine, wala Allah Mtukufu Hatakubali fidia, kutoka kwa hiyo nafsi, ya kuiyokoa na adhabu, wala hainufaiki kwa kuombewa na hakuna yoyote wa kuinusuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net