Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 125

وَإِذْ جَعَلْنَا ٱلْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَٱتَّخِذُوا۟ مِن مَّقَامِ إِبْرَٰهِـۧمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَآ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِىَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلْعَـٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ 125

(125) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akautaja mfano wa kudumu unaoonyesha uongozi wa Ibrahim. Nao ni Nyumba hii tukufu, ambayo amefanya kuikusudia kuwa nguzo ya Uislamu inayofuta madhambi na makosa. Na ndani yake zimo athari za Al-Khalil (Ibrahim) na kizazi chake, ambazo kwazo ulijulikana uongozi wake, na kukumbushwa kwazo hali yake, hivyo akasema: "Na kumbukeni tulipoifanya Nyumba ile (ya Alkaaba) iwe pahali pa kukusanyikia watu." Yani marejeo ambayo wanarejea huko ili kupata manufaa yao ya kidini na ya kidunia. Na wanarudirudi huko na wala hawamalizi huko haja zao. Na aliifanya "pahali pa amani." Kila mtu anapata amani ndani yake, hata mnyama mwitu, na hata vitu visivyo kuwa hai kama miti. Na ndiyo maana walikuwa - katika Jahiliyyah yao – pamoja na ushirikina wao – wakiiheshimu kwa heshima kubwa. Na mmoja wao akamkuta muuaji wa baba yake kwenye pahali patakatifu (Al-Haram) lakini hamsumbui. Na Uislamu ulipokuja, uliizidisha utakatifu, utukufu, cheo, na heshima. "Na alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapo ni sehemu inayojulikana sana ambayo sasa imetengenezwa mbele ya mlango wa Al-Kaaba, na kwamba kinachokusudiwa hapa ni zile rakaa mbili za baada ya kuzunguka Al-Kaba ambazo inapendekezwa kwamba ziwe nyuma ya Maqam Ibrahim (alipo kuwa akisimama Ibrahim). Na haya ndiyo maoni ya wengi wa wafasiri. Na inawezekana kwamba maqam ni ya (neno la) umoja lililounganishwa (na neno Ibrahim) basi likawa linajumuisha maeneo yote aliyosimama Ibrahim katika Hijja. Nayo ni Masha'ir (mambo takatifu) yote kama vile kuzunguka kando ya Al-Kaba, kufanya Sa'yi kati ya vilima vya Swafa na Marwa, na kusimama 'Arafa na Muzdalifah; na kurusha vijiwe kwenye Jamarat, na kuchinja na vitendo vinginevyo vya Hijja. Hivyo, inakuwa maana ya kauli yake "pawe pa kuswalia" yani mahali pa ibada. Yani mfuateni (Ibrahim) katika matendo takatifu ya Hijja. Na huenda maana hii ndiyo inayofaa zaidi kwa sababu maana ya kwanza inaigia humo, na kwa sababu neno hili linaweza kuwa na maana hii. "Na tulimwagiza Ibrahim na Ismail." yani tuliwateremshia wahyi na tukawaamrisha kuisafisha Nyumba ya Mwenyezi Mungu kutokana na ushirikina, ukafiri, maasia, na uchafu, najisi, na yasiyokuwa safi; ili iwe "kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kut'ufu" humo "na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu." Yani wanaoswali. Na alitaja Twawaf (kuzunguka kando ya Al-Kaba) kwanza kwa sababu ni mahsusi kwa Msikiti Mtakatifu. Kisha Itikafu kwa kuwa miongoni mwa masharti yake ni kwamba iwe msikitini tu. Kisha akataja swala ingawa ndiyo bora zaidi kwa hii maana (yani sio mahususi na Nyumba hii). Na Al-Bari (Muumbaji) aliiungaanisha Nyumba na nafsi yake kwa manufaa mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba, hilo linalazimu kujali kukubwa kwa Ibrahimu na Ismaili katika kuitakasa, kwa sababu ni nyumba ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wanafanya wawezavyo, na wanajitolea nguvu zao katika hilo. Miongoni mwake ni kwamba, huko kuunganisha kunalazimu heshima na kutukuza. Kwa hivyo, ndani yake kuna kuwaamrisha waja wake kuitukuza na kuiheshimu. Miongoni mwake ni kwamba, huku kuunganisha ndiyo sababu inayoleta nyoyo kwake.