Al-Baqara 2:116
البقرةوَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۖ بَل لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُۥ قَـٰنِتُونَ
Na ati wanasema: 'Mwenyezi Mungu ana mwana.' Subhanahu (ametakasika mbali na hayo!) Bali vyote vilivyomo mbinguni na duniani ni vyake. Vyote vinamdhalilikia Yeye kwa hofu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ati wanasema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu! Ametakasika na hayo. Bali vyote viliomo mbinguni na duniani ni vyake. Vyote vinamt'ii Yeye. [116]
[116] Basi huyo ambaye mambo yake ni kama hivi, na vyote viliomo ulimwenguni vinat'ii amri yake, vinanyenyekea kwa atakalo, basi Yeye huyo yuko juu mno, na mtukufu mno hata hahitajii kuwa na dhuriya au kujipa wana, kama wanavyo zua hawa Mayahudi na Wakristo na washirikina mapagani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema Mayahudi na Wanaswara, “Allah Mtukufu Amejifanyia mtoto.” kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, Kwani wote walioko mbinguni na ardhini ni milki Yake na ni watumwa Wake. Wote wanamnyenyekea Yeye na wanapelekewa wakiwa chini ya uendeshaji Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net