Al-Baqara 2:115
البقرةوَلِلَّهِ ٱلْمَشْرِقُ وَٱلْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا۟ فَثَمَّ وَجْهُ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ
Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kokote mnakoelekea, huko upo uso wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote mnako elekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa na Mjuzi. [115]
[115] Ikiwa washirikina waliwazuia Waislamu kusali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, hawatoweza kuwazuia kusali na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwani jiha zote na pande zote za dunia ni za Mwenyezi Mungu. Na hakika bila ya shaka Mwenyezi Mungu anampokelea Muislamu Sala zake, na anamkabili kwa radhi yake pande zote anapo fanya ibada yake. Kwani Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, hawadhikishi waja wake, na Yeye ni Mwenye kuijua vyema niya ya mwenye kumuelekea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zote pande mbili, upande wa kuchomoza jua na wa kuchwa kwake na vilivyo baina yake, ni vya Allah Mtukufu. Yeye ndiye Mmiliki wa ardhi yote. Basi pande wowote mnaouelekea kwenye Swala zenu kwa kuwa mmeamrishwa na Allah Mtukufu, Hakika nyinyi huwa mnaukusudia Uso Wake, hamkutoka kwenye ufalme Wake na utiifu wenu Kwake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye rehema za kuenea kwa waja Wake, ni Mjuzi wa vitendo vyao, hakuna chochote chenye kufichika Kwake Asikijue.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net