Al-Baqara 2:117
البقرةبَدِيعُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina mfano wa awali; na anapotaka jambo, basi Yeye kwa hakika huliambia tu: 'Kuwa!' Nalo huwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa. [117]
[117] Vipi awe na haja ya uzazi au atafute mwana huyo aliye anzisha kuumba Mbingu na Ardhi bila ya kuwa na kiigizo chochote kabla yake, na akavifanya vyote viliomo humo vimt'ii Yeye kwa kila atakalo, na visiweze kumuasi? Yeye akitaka kitu basi husema tu: Kuwa! Kikawa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Ndiye Muumba mbingu na ardhi, bila ya kuwa na mfano uliotangulia. Na Anapolikadiri jambo na Akataka liwe, huliambia, “Kuwa,” likawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net