Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 118

Al-Baqara 2:118

البقرة

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوْ تَأْتِينَآ ءَايَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَـٰبَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ

Maana

Na walisema wale wasiojua kitu: ʻMbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara.ʼ Kama hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii. Nyoyo zao zimefanana. Hakika Sisi tumeziweka wazi Ishara kwa watu wenye yakini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema wale wasio jua kitu: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara. Kama hivyo walisema wale walio kuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii. Nyoyo zao zimefanana. Hakika Sisi tumeziweka wazi Ishara kwa watu wenye yakini. [118]

[118] Washirikina wa Kiarabu walikakamia katika inadi yao kumfanyia Muhammad, wakamtaka kama wale kaumu zilizo tangulia zilivyo wataka Manabii wao. Wakasema kuwa hawatomuamini ila Mwenyezi Mungu aseme nao, na awaletee ishara, au muujiza wa kuuona utakao onesha ukweli wake. Haya ni kama walivyo sema Wana wa Israili kumwambia Musa: Hatukuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu na aseme nasi. Na kama masahaba (wanafunzi) wa Isa walipo mtaka awateremshie chakula kutoka mbinguni. Na haya yote ni kuwa nyoyo za makafiri na wapinzani wenye inda katika kila umma zimefanana. Haki haidhihiriki ila kwa wale ambao kuona kwao kumesafika, na akili zao zimeelekea kufuata Yakini, na kuitaka Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walisema wajinga miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo kumwambia Nabii na Mtume wa Allah Mtukufu Muhammad, rehema na amani zimshukie, kwa njia ya inadi, “Si aseme na sisi Allah Mtukufu moja kwa moja Atuambie kwamba wewe ni Mtume Wake au itujie miujiza itokayo kwa Allah Mtukufu yenye kuonyesha ukweli wako.” Neno kama hili walilisema ummah waliopita kuwaambia Mitume wao, kwa njia ya ukaidi na ujeuri, kwa sababu ya kufanana nyoyo za waliotangulia na waliofuata katika ukafiri na upotevu. Hakika Tumezifafanua aya kwa wale wanaoamini Imani ya kikweli, kwa kumuamini kwao Allah Mtukufu na kuzifuata kwao Sheria Alizowawekea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net