Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 116

وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۖ بَل لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُۥ قَـٰنِتُونَ 116

(116) "Na ati wanasema," yani Mayahudi, Wakristo, washirikina, na kila aliyesema hayo. "Mwenyezi Mungu ana mwana" Basi wakamhusisha na yale yasiyoufalia utukufu wake, na wakafanya kila ubaya, na wakazidhulumu nafsi zao. Na Yeye Mtukufu ana subira kwa hayo kutoka kwao, na akawafanya kuwa salama, na akawaruzuku pamoja na kumpunguzia kwao hadhi. "Ametakasika na hayo" yani yuko mbali na hayo, na ametakasika kutokana na kila waliyomueleza nayo washirikina na madhalimu, miongoni mwa yale yasiyofailia utukufu Wake. Basi ametakasika Yule ambaye ni Wake ukamilifu wote kwa namna yote, asiyepungukiwa hadhi kwa namna yoyote. Na pamoja na kujibu hiyo kauli yao, alisimamisha hoja na ushahidi juu ya kutakasika kwake na hilo, akasema: "Bali vyote vilivyomo mbinguni na duniani ni vyake" yani hivyo vyote ni miliki yake na watumwa wake. Anawaendesha kama anavyoendesha mmiliki wale anaowamiliki. Nao ni watiifu kwake, wamefanywa kuwa chini ya uendeshaji wake. Basi ikiwa wote ni waja wake wanaomhitaji, ilhali Yeye ni mwenye kujitosheleza hawahitaji wao, basi vipi atakuwapo yeyote miongoni mwao ambaye ni mtoto wake? Na mtoto ni lazima awe kutoka kwa sura ya baba yake, kwa sababu yeye ni sehemu yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mmiliki, Mwenye nguvu, nanyi ndio wamilikiwa wanaotawaliwa. Naye hamhitaji yeyote, nanyi ni wahitaji. Basi vipi pamoja na haya atakuwa na mwana? Hii ndiyo batili ya batili zote na yenye kuchukiza mno. Na Qunuut ni ya aina mbili: qunuut ya jumla, ambayo ni qunuut ya viumbe vyote chini ya kuendesha kwa Muumba, na qunuut maalumu, ambayo ni qunuut ya ibada. Na aina ya kwanza ni kama ilivyo katika Aya hii, nayo aina ya pili ni kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye Qunuut (wanyenyekevu). Kisha akasema: