Al-Kahf 18:71
الكهففَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِى ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْـًٔا إِمْرًا
Basi wawili hao wakatoka, hata walipoabiri jahazi (yule mtu), akalitoboa. (Musa) akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wawili hao wakatoka, hata walipo panda jahazi (yule mtu) akaitoboa. (Musa) akasema: Unaitoboa uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya. [71]
[71] Wakatoka wakitambaa na mfukwe wa bahari mpaka wakakuta jahazi wakaipanda. Yule mja mwema akaitoboa jahazi ile nayo imo safarini. Musa akapinga kwa kusema: Umeitoboa makusudi upate kuwazamisha watu wake? Ama hakika umefanya jambo ovu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakatoka kwenda kwenye ufuo wa Bahari, ikawapita mashua, wakawataka wenyewe wapande na wao. Walipopanda Al-Khiḍr aliukoboa ubao kutoka kwenye mashua na akaitoboa tundu. Mûsâ akamwaambia, Umeitoboa mashua ili uwazamishe wenyewe, na hali wao walituchukua bila malipo? Kwa hakika umefanya jambo baya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net