Al-Kahf
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِى ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْـًٔا إِمْرًا 71
{71} "Basi wawili hao wakatoka, hata walipopanda jahazi (yule mtu) akalitoboa." Yaani, Al-Khidhr akang'oa ubao mmoja, na alikuwa na lengo katika hayo, ambalo atakuja libainisha. Lakini Musa, amani iwe juu yake, hakuwa na subira juu ya hilo. Kwa sababu lilionekana kwa nje kuwa jambo ovu. Kwa sababu ni kutia dosari katika jahazi, na ni sababu ya kuzama kwa watu wake. Na ndiyo maana Musa akasema, “Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno." Na hili ni kutokana na kutokuwa na subira kwake, yeye amani iwe juu yake.