Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 70

Al-Kahf 18:70

الكهف

قَالَ فَإِنِ ٱتَّبَعْتَنِى فَلَا تَسْـَٔلْنِى عَن شَىْءٍ حَتَّىٰٓ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا

Maana

Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Basi ukinifuata usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia. [70]

[70] Yule mja mwema akasema: Basi ukinifuata na ukayaona usiyo yafahamu, usiingie kuniuliza mpaka nianze mimi kukusimulia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Al-Khiḍr akakubali na akamwambia, «Ukifuatana na mimi usiniulize juu ya chochote usichokikubali mpaka nikupe maelezo yake yaliyofichika kwako bila ya wewe kuuliza».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net