Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 69

Al-Kahf 18:69

الكهف

قَالَ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ صَابِرًا وَلَآ أَعْصِى لَكَ أَمْرًا

Maana

Akasema: In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akitaka), utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mvumilivu, wala sitoasi amri yako. [69]

[69] Musa akasema: Inshallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mimi ni mwenye kusubiri, na mt'iifu kwako kwa yote utayo niamrisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsâ akamwambia, «Utanikuta, Allah Mtukufu Akitaka, ni mwenye kuvumilia kwa nitakayoyaona kwako, na sitaenda kinyume na amri yako yoyote utakayoniamrisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net